Search

Saved articles

You have not yet added any article to your bookmarks!

Browse articles

GDPR Compliance

We use cookies to ensure you get the best experience on our website. By continuing to use our site, you accept our use of cookies, Privacy Policy, and Terms of Service.

Binti Mwenye Kichanga Azimiwa Simu Baada ya Kufika Dar es Salaam

Msichana aitwaye Esters (25) mwenye mtoto mchanga wa miezi mmoja na nusu kutoka Songwe amejikuta katika wakati ngumu baada ya kuzimiwa simu na mwenyeji wake ambaye ni baba wa mtoto baada ya kufika stendi ya Magufuli, Dar es Salaam.

Ester ambaye alikuwa anauza uji ili kujikimu na maisha kabla ya kupata ujauzito, amesema alikubaliana na Baba mtoto wake huyo ambaye ni dereva wa malori kwamba akifika Dar es Salaam atapewa mtaji wa kuuza nguo za ndani ili aweze kijikimu kiuchumi.

Baada ya kukaa mpaka jioni hii, alienda Ustawi wa Jamii ambapo alipewa barua ya kupeleka kwa trafiki ili arejee nyumbani huku akidai licha ya kupata msaada huo hana hata hela ya chakula kwa leo na ananyonyesha.

“Nimebakiwa na buku tu, sijala toka asubuhi na ninanyonyesha. Mungu atanisaidia na mtoto atakuwa,” alisema Ester ambaye ni Mama wa mtoto mmoja aitwaye Ester.

 

 

 

Chanzo; Bongo 5

Kuhusiana na mada hii: