Wakati kesi ya uhaini inayomkabili mchungaji Godfrey Malisa ikipangwa kutajwa tena Januari 16,2025, imebainika kuwa upande wa Jamhuri imemfungulia kesi nyingine ya Jinai inayohusiana na makosa ya kimtandao.
Kesi ya uhaini namba 000028333 ya 2025 ilitajwa jana Januari 2,2026 mbele ya Hakimu Mkuu Mkazi Ally Mkama wa Mahakama ya Hakimu Mkazi Moshi lakini ikaahirishwa hadi Januari 16,2026 kwa kuwa upelelezi wake haujakamilika.
Katika kesi hiyo nyingine namba 000028411 ya 2025, Malisa anatuhumiwa kuchapisha taarifa kwenye mtandao wake wa Youtube, akimdai Rais Samia Suluhu Hassan, anatakiwa kujiuzulu kwa kusimamia mauaji ya maelfu ya watanzania.
Chanzo; Mwananchi