Search

Saved articles

You have not yet added any article to your bookmarks!

Browse articles

GDPR Compliance

We use cookies to ensure you get the best experience on our website. By continuing to use our site, you accept our use of cookies, Privacy Policy, and Terms of Service.

Sababu za Mchina Kumburuza DPP, IGP Mahakamani

Raia wa China, Xiuzhu Yan amewasilisha maombi kortini (Habeas Corpus) dhidi ya Inspekta Jenerali wa Polisi (IGP) na Mkurugenzi wa Mashitaka Nchini (DPP), kupinga kushikiliwa mahabusu kwa siku 82 tangu Novemba 2025.

Katika maombi hayo namba 000002421 ya 2026, Yan anayewakilishwa na wakili Michael Lugina, amemuunganisha Mkurugenzi wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru) na Kamanda wa Polisi (RPC) Kanda Maalum ya Dar es Salaam.

Wajibu maombi wengine katika maombi hayo ambayo yamewasilishwa chini ya ombi la usikilizwaji wa haraka (extreme urgency), ni pamoja na Mkuu wa Polisi wa wilaya (OCD) na Mkuu wa Kituo (OCS) katika mahabusu anakoshikiliwa.

Maombi hayo yamefunguliwa Februari 4,2026 katika Mahakama Kuu ya Tanzania Kanda ya Dar es Salaam na yamepangwa kutajwa Februari 10,2026 saa 4:00 asubuhi mbele ya Jaji Salma Maghimbi wa Mahakama hiyo jijini Dar es Salaam.

Tangu Novemba 14, 2025 hadi maombi hayo yanafunguliwa Februari 4, 2026, raia huyo alikuwa amefikisha siku 82 akiwa mahabusu kwa tuhuma ambazo hazikuelezwa katika kiapo cha wakili Lugina, kilichoambatanishwa na maombi.

 

 

Chanzo; Mwananchi

Kuhusiana na mada hii: