Kamanda wa Polisi mkoa wa Kilimanjaro Kamishna Msaidizi Mwandamizi (SACP) Simon Maigwa amesema takribani vijana 300 waliokuwa wakishikiliwa na jeshi hilo kutokana na vurugu za uchaguzi wameachiwa.
Amesema bado jeshi hilo linawashikilia vijana 9 ambao baada ya mchujo, ushahidi umeonesha walishiriki kwenye vitendo vya kihalifu na kueleza kuwa watafikishwa mahakamani kusomewa mashtaka yanayowakabili.
Chanzo; Global Publishers