Search

Saved articles

You have not yet added any article to your bookmarks!

Browse articles

GDPR Compliance

We use cookies to ensure you get the best experience on our website. By continuing to use our site, you accept our use of cookies, Privacy Policy, and Terms of Service.

Majaliwa Atoa Maelekezo Suasua ya Huduma Mabasi Mwendokasi

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa ametembelea vituo vikubwa vya Mwendokasi vilivyopo Barabara ya Morogoro, Kivukoni na Kimara na kucanya ukaguzi wa vituo hivyo ili kujua changamoto hasa inayofanya huduma hizo kusuasua.

Majaliwa ametoa maelekezo kwa uongozi mpya unaosimamia huduma ya mabasi hayo na kuwaambia kuwa huduma hiyo ni muhimu hivyo umakini unahitajika kwenye kuwahudumia Watanzania hasa kwenye kuzingatia muda.

Ikiwa ni saa 24 zimepita tangu Mkuu wa Mkoa huo, Albert Chalamila alipotembelea eneo la Kimara ambalo linatajwa kuwa na adha kubwa huku akiwaomba wananchi kuwa wavumilivu kwani changamoto hiyo inaelekea kupatiwa ufumbuzi tayari mabasi ya kampuni ya Mofat yamepelekwa kwenda kuongeza nguvu kwenye njia hiyo.

Waziri Mkuu ametoa maelekezo hayo ikiwa ni saa chache baada ya taarifa iliyotolewa leo Alhamisi Oktoba 2, 2025 na Katibu Mkuu Kiongozi, Dk Moses Kusiluka, ikieleza uteuzi na utenguzi alioufanya Rais Samia akimteua Said Tunda kuwa Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Mabasi Yaendayo Haraka (DART).

Tunda anachukua nafasi ya Dk Athumani Kihamia ambaye uteuzi wake umetenguliwa kuanzia leo Oktoba 2, 2025. Pia, Rais Samia amemteua Pius Ng’ingo kuwa Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni ya Mabasi Yaendayo Haraka (UDART), akichukua nafasi ya Waziri Kindamba, ambaye uteuzi wake pia umetenguliwa. Taarifa ya uteuzi na utenguzi huo imetolewa wakati Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akifanya ziara kwenye kituo cha mwendokasi cha Kivukoni na baadaye Kimara leo.

 

Chanzo: Mwananchi

Kuhusiana na mada hii: