Search

Saved articles

You have not yet added any article to your bookmarks!

Browse articles

GDPR Compliance

We use cookies to ensure you get the best experience on our website. By continuing to use our site, you accept our use of cookies, Privacy Policy, and Terms of Service.

ACT Wapinga Uteuzi Wajumbe Tume ya Uchaguzi

Chama cha ACT Wazalendo kimetangaza kuikataa Tume ya Uchunguzi iliyoundwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan kuchunguza matukio ya Oktoba 29, 2025 na siku zilizofuatia, kikisema kuwa tume hiyo haina sifa ya kuleta ukweli, uwazi wala haki kwa waathirika.

Mapema, leo Jumanne, Novemba 18, 2025, Rais Samia ametangaza majina ya wajumbe saba wa tume hiyo akiwemo Jaji Mkuu mstaafu, Profesa Ibrahim Juma; Katibu Mkuu Kiongozi mstaafu, Balozi Ombeni Sefue;
Mwanadiplomasia Balozi Radhia Msuya; pamoja na Balozi Paul Meela.

Wengine ni Mkuu wa Jeshi la Polisi mstaafu, Said Ally Mwema; Balozi David Kapya; na Waziri wa zamani wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa, Dk Stergomena Tax.

Kwa mujibu wa Ikulu, hatua ya kuteua tume hiyo ni utekelezaji wa ahadi ya Rais Samia aliyoitoa Novemba 14, 2025 wakati akizindua Bunge la 13 jijini Dodoma, alipoeleza kusikitishwa kwake na matukio hayo na kuahidi kuyachunguza.

Matukio ya Oktoba 29 na siku zilizofuata yalitokea katika mikoa mbalimbali nchini ikiwemo Dar es Salaam, Mwanza, Mbeya, Songwe, Geita, Arusha, Mara na Ruvuma na yalisababisha vifo vya raia, majeruhi wengi, uharibifu wa mali za watu binafsi na miundombinu ya umma.

Hata hivyo, ACT Wazalendo imesema tume hiyo ni “dhihaka kwa waliopoteza maisha, majeruhi na familia zilizofiwa,” ikieleza kuwa baadhi ya wajumbe ni watu wanaotoka katika taasisi ambazo zinapaswa kuchunguzwa badala ya kupewa jukumu la kuchunguza.
Kupitia taarifa iliyosainiwa na Katibu Mkuu wa Chama hicho, Ado Shaibu imeeleza kuwa hataweza kuipa uhalali tume hiyo.

“Hatuwezi kuipa tume hii uhalali kwa sababu imeundwa na watu ambao taasisi zao zinadaiwa kuhusika moja kwa moja katika tukio lenyewe. Huu si utaratibu wa kutafuta ukweli, huu ni utaratibu wa kulinda wahusika,” ameeleza Ado kupitia taarifa hiyo na kuongeza kuwa: “Hakuna familia iliyoathirika, hakuna mwananchi yeyote mwenye kiu ya haki atakayeiambia tume hii ukweli wake halisi. Hii si tume huru na kwa mantiki hiyo haiwezi kuleta haki,”.

 

Chanzo; Mwananchi

Kuhusiana na mada hii: