Search

Saved articles

You have not yet added any article to your bookmarks!

Browse articles

GDPR Compliance

We use cookies to ensure you get the best experience on our website. By continuing to use our site, you accept our use of cookies, Privacy Policy, and Terms of Service.

Muinjilisti Jela Miaka 30 Kwa Kubaka Mtoto wa Mwaka Mmoja

Tanga, Mahakama ya Wilaya ya Pangani, tarehe 10 Septemba 2025 imetoa hukumu ya kifungo cha miaka 30 jela kwa mtuhumiwa Grayson Muze Msemo (55), Mkristo, Muinjilisti na mkazi wa Raskazoni, baada ya kukutwa na hatia ya kosa la kubaka mtoto mwenye umri wa mwaka 1 na miezi 4. Ambapo,  mtuhumiwa alitenda kosa hilo tarehe 1 Septemba 2025 katika eneo la Funguni Street, Pangani.

Hukumu ikisomwa Septemba 10,2025 , Mheshimiwa Husna Mwiula, Hakimu Mkazi wa Mahakama ya Wilaya ya Pangani, alisema kuwa mahakama imeridhika na ushahidi uliowasilishwa na kumhukumu mtuhumiwa kifungo cha miaka 30 jela ili iwe fundisho kwa jamii na kuhakikisha haki inatendeka.

 

Chanzo: Polisi Tanzania

Kuhusiana na mada hii: