Search

Saved articles

You have not yet added any article to your bookmarks!

Browse articles

GDPR Compliance

We use cookies to ensure you get the best experience on our website. By continuing to use our site, you accept our use of cookies, Privacy Policy, and Terms of Service.

Waandishi Wafunza Kuandika Habari za Ushahidi

Waandishi wa habari wametakiwa kuhakikisha wanaandika habari zenye ushahidi na ushawishi wa kisera, ili zilete manufaa kwa jamii hasa wakati wa mabadiliko ya tabianchi.

Hayo yamesemwa na Kiongozi wa kimataifa wa haki ya tabianchi katika kukuza haki za kijamii (ActionAid) Dk. Teresa Anderson leo Februali 12 wakati akitoa mada ya matokeo ya COP30 kuhusu mpito wa haki kwenye mafunzo ya mabadiliko ya tabianchi na athari za jinsia.

Mafunzo hayo yameshirikisha wanahabari kutoka nchi sita za Afrika na kufanyika kwa njia ya mtandao ulioandaliwa na shirika la Media for Environment, Science, Health and Agriculture (MESHA) kwa kushirikiana na kituo cha kimataifa cha utafiti kwa maendeleo cha nchini Canada (IDRC.CRDI)

Dk. Anderson anasema wanahabari wanapaswa kuandika habari zenye kuleta mabadiliko kwa jamii, ziwe na ushawishi wa kisera badala ya kuwa taarifa za kawaida kwa jamii.

Anasema lengo la mafunzo hayo ni kuimarisha uandishi wa habari za sayansi, mazingira, afya na kilimo kwa kutumia ushahidi na data sambamba na kuandika habari za kina na za uwajibikaji kuhusu mabadiliko ya tabianchi, matumizi sahihi ya data na tafiti za kisayansi, pamoja na kufuatilia utekelezaji wa sera na ahadi za serikali. .

Mshiriki wa mafunzo hayo Afidh Kido kutoka Tanzania anasema mafunzo hayo yana umuhimu kwa wanahabari, hasa katika nyakati hizi za mabadiliko ya tabianchi yanapaswa kutolewa mara kwa mara ili kuwafanya wanahabari kutambua faida na hasara za mabadiliko hayo na kuelimisha umma kwa kina.

Mshiriki mwingine kutoka nchini Kenya Agakan Goki anasema masuala ya mabadiliko ya tabianchi na jinsia yanapaswa kupewa kipaumbele kihabari,ili kuelimisha jamii ambayo imekuwa ikilalamikia mabadiliko hayo bila kujua kama nayo yanachangia hali hiyo.

 

 

Chanzo; Nipashe

Kuhusiana na mada hii: