Search

Saved articles

You have not yet added any article to your bookmarks!

Browse articles

GDPR Compliance

We use cookies to ensure you get the best experience on our website. By continuing to use our site, you accept our use of cookies, Privacy Policy, and Terms of Service.

Mwigulu Ahadi Kufyeka Wavivu, Wala Rushwa Tanzania

Waziri Mkuu mteule Dkt. Mwingulu Nchemba amesema kuwa licha ya Tanzania kuwa tajiri lakini bado asilimia 8% ya Watanzania wanaishi kwenye umaskini wa kupindukia na asilimia 26% ya Watanzania wanaishi kwa mlo mmoja ambapo amesisitiza kuwa maisha ya Umaskini hajayasoma kwenye kitabu bali ameyaishi Kijijini kwa takribani miaka 32.

Dkt. Nchemba ameyasema hayo hii leo Novemba 13, 2025 baada ya Kuthibitishwa na Wabunge wa Bunge la Jamhuri ya Muungano kuwa Waziri Mkuu ambapo amesema kuwa akiwa kama Waziri Mkuu atahakikisha kuwa kila Mtanzania anahudumiwa kwa heshima katika taasisi za Serikali na atahakikisha wavivu wote na watumishi wote wa uma wenye kauli mbovu kwa watanzania wanashughulikiwa.

“Mimi Umaskini wa Watanzania Sijausoma kwenye vitabu nimeuishi, Mheshimiwa Spika katika maisha yangu haya na Umri wangu huu miaka takribani 32 nimeishi katika maisha hayo ya umaskini nimeishi katika maisha ambayo nilikuwa najifunika nguo aliyokuwa anajifunga shemeji yangu hivyo kwa kuzingatia kazi kubwa iliyopo mbele yetu”

“Watumishi wa Umma na Watanzania wote lazima twende kwa gia ya ya kupandia Mlima, lazima twende na gia ya kupita kwenye bahari yenye mawimbi na anga lenye mawingu chombo kifike salama na watu wake wakiwa salama hivyo watumishi wote wa Umma walio wavivu, wazembe, wala rushwa na wenye lugha mbaya kwa Watanzania tuwe tayari nitakuja na fyekeo na rato lazima maono ya Mheshimiwa Rais yatekelezwe. ” Amesema Dkt. Mwigulu Nchemba

 

Chanzo; Millard Ayo

Kuhusiana na mada hii: