Leo September 25, 2025, Ambapo Jana Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam, Albert Chalamila ameagiza Kampuni zote za udalali hususani zinazotumika na Mahakama, kuacha mara moja kuwatumia Mabaunsa wakati wa kukomboa madeni na kutoa vitu vya Watu nje akisema Mabaunsa hao hawana utaalamu wa kazi hiyo na wanalalamikiwa kunyanyasa Watu, kuiba vitu, kujeruhi na hata kubaka.
Chalamila amesema hayo baada ya kufika Mikocheni kukutana na Alice Haule, Mjane wa Marehemu Justice Rugaibula ambaye juzi amevamiwa kwenye nyumba yake na Mabaunsa waliodai kuwa wametumwa na Mfanyabiashara Mohamed Yusufali ambaye kwa muda mrefu wamekuwa wakivutana na Alice kisheria Mahakamani kwa kesi tofauti za madai hata kabla ya Mumewe kufariki.
Kupitia Leo Tena ya Clouds Fm, Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni Mheshimiwa Saad Mtambule, amefunguka mambo mbalimbali kuhusiana na sakata hilo ikiwemo Mabaunsa wanne kushikiliwa.
Chanzo; Clouds Media