Kufuatia picha mjongeo zilizosambaa ambazo zinaonesha tukio la watu kumpiga kijana mdogo na kumuua kisha kumchoma moto wakimtuhumu kuiba parachichi kusambaa kwenye mitandao ya kijamii, Serikali mkoani Iringa ikiongozwa na Mkuu wa mkoa huo, Kheri James kwa kushirikiana na vyombo vya ulinzi na usalama wamechukua hatua za haraka ambapo tayari wahusika wote wa mauaji hayo wamekamatwa na wapo mikononi mwa Jeshi la Polisi kwa mahojiano zaidi.
Mkuu wa mkoa wa Iringa, Kheri James ametembelea eneo la tukio ikiwa ni pamoja na nyumbani kwa marehemu eneo la Don Bosco Manispaa ya Iringa kwa lengo la kutoa neno la pole kwa ndugu wa marehemu na kuzungumza na jamii ya eneo hilo.
Aidha, video mjongeo hizo zilianza kutanda kwa kasi ndani ya mitandao ya kijamii mapema Septemba 13,2025 zikionyesha watu kadhaa wakimshambulia wa malungu kijana huyo ambapo badae kidogo Jeshi La Polisi likatoa taarifa kwa umma dhidi ya tukio hilo wakidai kulifatilia kiundani.
Chanzo; Wasafifm