Mahakama Kuu Masjala Ndogo Dar es Salaam imetoa hati ya wito wa kufika mahakamani hapo kwa Mkuu wa Jeshi la Polisi Nchini (IGP) na wenzake watano, kuhusiana na sakata la kushikiliwa kwa Makamu Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) Tanzania Bara, John Heche.
Mahakama hiyo imetoa wito huo kufuatia shauri la maombi lililofunguliwa mahakamani hapo na mawakili wa Chadema kwa niaba ya Heche, wakiomba amri ya Mahakama kuwataka wajibu maombi kumfikisha mahakamani kiongozi huyo au limwachie kwa dhamana.
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Mkurugenzi wa Sheria na Haki za Binadamu wa Chadema, Wakili Gaston Garubindi, shauri hilo limesajili Mahakama Kuu Masjala Ndogo Dar es Salaam na limepangiwa kusikilizwa na Jaji Obadia Bwegoge.
Chanzo; Mwananchi