Search

Saved articles

You have not yet added any article to your bookmarks!

Browse articles

GDPR Compliance

We use cookies to ensure you get the best experience on our website. By continuing to use our site, you accept our use of cookies, Privacy Policy, and Terms of Service.

Samia Akisikia Kilio cha Wamachinga Kusogea Jangwani

Rais wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan, amesema amesikia sauti za Vijana na amewahakikishia kuwa soko la Jangwani litajengwa pale utakapokamilika ujenzi wa daraja la Jangwani.

Rais Samia amesema hayo leo February 08,2026 wakati akizindua soko la Kariakoo.

“Na leo hapa niliambiwa kuna Wanangu Wamachinga ambao walitaka kuingia na fulana zao waniambie Mama tunasubiri soko la kule Jangwani lakini mmewazuia kuingia nataka niwaambie Wanangu sauti zenu nimezisikia na soko lile tupo katika hatua ya kulijenga”

“Kuna mambo yanafanyika tuweke bonde sawa tujenge soko, Serikali ipo tayari kujenga soko tukishajenga daraja, sauti zenu nimezisikia soko tutalijenga Jangwani”

 

 

Chanzo; Millard Ayo

Kuhusiana na mada hii: