Kesi ya uhaini inayomkabili Tundu Lissu inaendelea katika Mahakama Kuu baada ya kuahirishwa hadi saa tano asubuhi.
Kuahirishwa huko kulikuja baada ya Lissu kudai kuwa baadhi ya wanachama wa chama chake walizuiwa kuingia mahakamani.
Hata hivyo, majaji wanaosikiliza shauri hilo walisema hakuna taarifa yoyote inayoonyesha kuwa wanachama wa Chadema walizuiwa. Walibainisha kuwa kuna utaratibu maalumu wa kuingia mahakamani unaozingatia idadi ya watu, lakini hakuna zuio lolote dhidi ya wanachama.
Awali, viongozi wa Chadema walimshinikiza Lissu asikubali kesi kuendelea hadi pale ambapo utaratibu wa kuingia kwa wanachama wao ungepitiwa upya.
Chanzo; Bongo 5