Search

Saved articles

You have not yet added any article to your bookmarks!

Browse articles

GDPR Compliance

We use cookies to ensure you get the best experience on our website. By continuing to use our site, you accept our use of cookies, Privacy Policy, and Terms of Service.

Watatu Wadakwa kwa Utapeli wa Zaidi ya Milion 140

Jeshi la Polisi Mkoa wa Ruvuma linawashikilia watuhumiwa watatu kwa tuhuma za utapeli wa shilingi 147,300,000.

Tukio hilo lilitokea Februari 5, 2026, Bombambili, Songea, ambapo wakala wa CRDB, Paulo Dainet Akwezo, alilaghaiwa na watu waliomshawishi kuwa wanaweza kuziongeza fedha zake kwa njia za kishirikina.

Inadaiwa wakala huyo alikusanya fedha hizo kutoka kwa mawakala wenzake kwa madai ya kuweka salio (float) benki, lakini badala yake alizipeleka katika nyumba ya kulala wageni alikoelekezwa ambapo aliambiwa azitandaze pesa hizo kitandani, kisha azipake mafuta na aondoke katika chumba hicho bila kukifunga ili malaika waweze kuzichukua pesa hizo na kuzirejesha zikiwa zimeongezeka zaidi ya hapo awali. Wakala huyo alitekeleza maagizo hayo kwa kuondoka. Baada ya saa moja, alirudi katika chumba hicho na kukuta pesa zote hazipo. Akaamini kuwa malaika wamezichukua. Aliendelea kukaa chumbani humo kwa muda mrefu akisubiri pesa zirudi, lakini hazikurudi mpaka mwajiri wa wakala huyo alipopata taarifa na kutoa taarifa kituo cha Polisi.

Polisi walianza uchunguzi na Februari 17 na 18, 2026 waliwakamata watuhumiwa watatu katika maeneo ya Dodoma na Mbinga. Watuhumiwa watafikishwa mahakamani kwa hatua zaidi za kisheria.

 

 

Chanzo; Wasafi Media

Kuhusiana na mada hii: