Mjumbe wa Kamati Kuu ya CHADEMA, Godbless Lema anadaiwa kukamatwa Jijini Arusha na jeshi la polisi ikiwa ni siku moja tangu jeshi hilo kutoa wito kwa baadhi ya viongozi wa chama hicho kujisalimisha kwa jeshi hilo kwa tuhuma zinazohusiana na vurugu na maandamano wakati wa Uchaguzi Mkuu Oktoba 29.
Taarifa ya kukamatwa kwa kiongozi huyo imetolewa na Katibu wa CHADEMA Kanda ya Kaskazini, Ndonde Totinan ambaye ameeleza kuwa Lema amekamatwa eneo la Usa River mkoani Arusha.
Katika orodha ya viongozi wa CHADEMA wanaotakiwa kujisalimisha polisi kwa mujibu wa taarifa ya jeshi hilo ya Novemba 7, mbali na Lema yumo John Mnyika, Deogratius Mahinyila, Hilda Newton, Brenda Rupia, Award Kalonga, Boniface Jacob, Amani Golugwa na Machumu Kadutu.
Chanzo; Nipashe