Search

Saved articles

You have not yet added any article to your bookmarks!

Browse articles

GDPR Compliance

We use cookies to ensure you get the best experience on our website. By continuing to use our site, you accept our use of cookies, Privacy Policy, and Terms of Service.

TAKUKURU Waokoa Bilioni 60, Kesi 489 Mahakamani

Mkurugenzi Mkuu wa TAKUKURU Crispin Francis Chalamila amesema katika kipindi cha Julai hadi Disemba mwaka jana, wameweza kuokoa shilingi bilioni 60.2 kutokana na kudhibiti vitendo vya rushwa huku kati ya kesi 489 za rushwa zilizofikishwa Mahakamani katika kipindi kifupi Jamhuri ikishinda kwa asilimia 68.8.

Waziri Mkuu Dkt Mwigulu Lameck Nchemba amepongeza mafanikio hayo akisema ni kazi nzuri ambayo Watanzania wanatamani kusikia na kwamba hata Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan aliagiza tuhuma za rushwa kuhakikishwa zinafikishwa mamlaka sahihi, zinachunguzwa mara moja, uchunguzi unakamilika na mashauri yanafikishwa Mahakamani ili haki itendeke.

Akasema fedha zilizookolewa na TAKUKURU zimetumika kwa afua zingine za maendeleo ikiwemo afya ya mama na mtoto, vifaa tiba, miundombinu na maendeleo mengine.

 

 

Chanzo;  Itv

Kuhusiana na mada hii: