Search

Saved articles

You have not yet added any article to your bookmarks!

Browse articles

GDPR Compliance

We use cookies to ensure you get the best experience on our website. By continuing to use our site, you accept our use of cookies, Privacy Policy, and Terms of Service.

Luku Kuisha Haraka Tanesco Yabaini Mifumo Mibovu ya Umeme Majumbani

Kufuatia malalamiko ya wateja wa umeme wa Luku kuisha haraka katika matumizi, Shirika la Umeme Tanzania (Tanesco) limefanya ukaguzi wa kitaalamu na kubaini, tatizo hilo linasababishwa na mifumo mibovu ya umeme.

Baada ya kupokea malalamiko hayo, Tanesco, iliwalazimu kufanya ukaguzi wa kitaalamu katika baadhi ya nyumba ili kubaini chanzo cha tatizo hilo.

Matokeo ya awali yanaonesha kuwa, katika matukio mengi, tatizo siyo mita za umeme, bali ni mifumo mibovu ya umeme (wiring) majumbani.

Pia, kukosekana kwa elimu sahihi ya matumizi ya umeme na uharibifu wa mifumo ya umeme katika nyumba nyingi, kumetajwa kuwa chanzo cha ongezeko la matumizi ya umeme, ajali za moto na upotevu wa mali na maisha.

Akizungumza leo Januari 27, 2026 baada ya kufanya uchunguzi katika nyumba zilizowasilisha malalamiko, mhandisi wa Tanesco, Ally Mbonde amesema wamefanya uchunguzi katika baadhi ya nyumba na kubaini kuwa, mita nyingi ziko salama na zinapima kwa usahihi.

 

 

Chanzo; Mwananchi

Kuhusiana na mada hii: