Search

Saved articles

You have not yet added any article to your bookmarks!

Browse articles

GDPR Compliance

We use cookies to ensure you get the best experience on our website. By continuing to use our site, you accept our use of cookies, Privacy Policy, and Terms of Service.

Serikali Kushawishi Makampuni ya Simu Kushusha Gharama Vifurishi vya Simu

Serikali imeahidi ikuendelea kuzungumza na taasisi binafsi zinazotoa huduma za simu kupunguza zaidi gharama za vifurushi ili kufikia uchumi wa kidigiti.

Naibu Waziri wa Mawasiliano na Teknolojia ya Habari Dk. Switbert Mkama aeleza hayo leo Dodoma wakati akijibu swali la nyongeza la Mbunge wa Momba (CCM) Condester Sichalwe.

Katika swali lake Sichalwe alitaka kujua mkakati wa serikali kukaa na watoa huduma za intaneti kutoka taasisi binafsi kwa ajili ya kupunguza gharama za vifurushi.

Dk.Mkama amesema serikali inatambua umuhimu wa upatikanaji wa huduma za mawasiliano kwa gharama nafuu kwa wananchi.

“Kwa sasa ukiondoa nchi ya Rwanda Tanzania ndio nchi yenye vifurushi nafuu zaidi kuliko nchi nyingine,” amesema.

 

 

Chanzo; Nipashe

Kuhusiana na mada hii: