Rais wa Jamhuri wa Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan, akilihutubia Bunge la Jamhuri wa Muungano wa tanzania kwa mara ya kwanza baada ya Uchaguzi Mkuu uliofanyika Oktoba 29, 2025 ameagiza vijana waliokamatwa siku ya maandamano na kushtakiwa kwa makosa ya uhaini
kuachiwa “ Vijana wamekamatwa kushtakiwa kwa makosa ya uhaini hawakujua wanachokifanya, wengine wamefuata mkumbo, nikiwa kama Mama nanielekeza vyombo vya kisheria kuangalia makosa yaliyofanywa na Vijana wetu, kwa wale ambao walifanya mambo kwa kufuata mkumbo na hawakudhamiria kufanya uhalifu wafutie makosa yao”
“Ukiangalia clip zile za maandamano unaona kabisa kuna Vijana waliingia kwa kufuata mkumbo, wanaimba kwa ushabiki, naelekeza Ofisi ya DPP kuchuja viwango vya makosa na kwa waliofuata mkumbo wawaachie waende kwa Wazazi wao” Rais wa Jamhuri wa Muungano wa Tanzania Samia Suluhu kwenye Bunge la 13.
Aidha, akilifungua Bunge la 13 Rais Samia, ameliongoza kwa maombi kuwaombea wale wote waliopoteza maisha kipindi cha vurugu ambazo zilianza Oktoba 29, na kutuma salamu za pole kwa waliopoteza wapendwa wao.
Chanzo; Tanzania Journal