Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan ametoa onyo kali kwa wanaoshikwa masikio au kushawishiwa kuvunja amani ya Nchi waache mara moja na kusisitiza kuwa tofauti za mawazo ni jambo la kawaida lakini hazipaswi kutugawa wala kuharibu utulivu wa nchi.
Akizungumza leo Ijumaa, Januari 9, 2025, wakati wa uzinduzi wa Hoteli ya Jaz Elite Aurora iliyopo Michamvi, Mkoa wa Kusini Unguja, Zanzibar, Rais Samia amesema amani, usalama na utulivu wa nchi ndiyo kivutio kikubwa kwa wawekezaji.
Chanzo; Bongo 5