Profesa Anna Tibaijuika ambaye ni Waziri wa zamani wa Ardhi, Nyumba na Makazi katika Serikali ya awamu ya nne chini ya Dr. Jakaya Kikwete, ametuma salamu za pole kwa Watanzania wote waliofikwa na madhara ya maandamano ya October 29 na kushauri kwamba wote waliofariki wazikwe kwa heshima.
Kupitia ukurasa wake wa X, Profesa Tibaijuka pia amewaomba kuendelea kuwafariji Wafiwa wote pamoja na kuwapa misaada mbalimbali katika kipindi hiki kigumu ambacho wamepoteza Wapendwa wao.
“UCHAGUZI 29 OKTOBA ee Mungu tunawaombea Marehemu wetu raha ya milele, tuwazike kwa heshima, kuwafariji Wafiwa, kuuguza Majeruhi, kusaidia Waathirika, tuombe toba kuondosha sifa za Taifa letu kwa kutotambua HAKI ndiyo msingi wa yote na haina mbadala, twakuomba utusikie” - ameandika Profesa Tibaijuka.
Chanzo; Millard Ayo