Mwili wa Mtanzania Joshua Loitu Mollel umeagwa na kuzikwa leo wilayani Simanjiro, mkoani Manyara, baada ya mabaki yake kurejeshwa nchini kutoka Israel.
Joshua aliuawa Oktoba 7, 2023, katika tukio lililoripotiwa na vyombo vya habari vya kimataifa.
Maziko hayo yalihudhuriwa na viongozi wa serikali, viongozi wa dini, wananchi pamoja na mwakilishi wa ubalozi wa Israel nchini. Familia, ndugu, jamaa na marafiki walijitokeza kwa wingi kumuaga kijana huyo aliyekwenda Israel kushiriki mafunzo ya kilimo.
Chanzo; Wasafi Media