Wabunge wamemaliza uchaguzi wao leo kwa kumchagua aliyepata shida ya kuzungumza lugha ya Kiingereza alipokuwa akiomba kura kuwania nafasi ya uwakilishi kwenye Bunge la Dunia,
Mbunge huyo wa Ukonga kupitia Chama cha ACT-Wazalendo, Bakari Shingo alishindwa kujieleza kwa lugha ya Kiingereza wakati akiomba nafasi hiyo ambayo alikuwa mgombea pekee.
Uchaguzi huo umefanyika leo Alhamisi Februari 5, 2026, wakati wa kujieleza kulizuka vitimbwi kwa baadhi ya wabunge hasa kwenye lugha ya kiingereza, ambayo ilikuwa kigezo kilichotangazwa kwa waombaji.
Hata hivyo, mbunge huyo ameshinda kwenye nafasi hiyo ya Jukwaa la Mabunge ya Maziwa Makuu.
Chanzo; Millard Ayo