Search

Saved articles

You have not yet added any article to your bookmarks!

Browse articles

GDPR Compliance

We use cookies to ensure you get the best experience on our website. By continuing to use our site, you accept our use of cookies, Privacy Policy, and Terms of Service.

Lissu Apinga Utaratibu Shahidi wa Nne, Afichwa Kwenye Boksi

Mwenyekiti wa CHADEMA Tundu Lissu amepinga utaratibu wa Shahidi wa nne wa Upande wa Jamhuri kutoa ushahidi akiwa ndani ya kiboksi maalumu katika Mahakama Kuu ya Tanzania, Masijala Ndogo ya Dar es Salaam ambapo Lissu alidai kuwa Shahidi huyo anatakiwa kusimama kwenye kizimba cha kawaida kama inavyoelekezwa na sheria na siyo kujificha katika kifaa kisichoonekana na Mahakama huku ikisikika sauti yake pekee.

Kesi hiyo ilipangwa leo mbele ya Jopo la Majaji watatu akiwemo Jaji Dunstan Ndunguru kwa ajili ya kuendelea na ushahidi ambapo Lissu alieleza kuwa amri ya ulinzi wa Mashahidi iliyotolewa Julai 2025 haikutoa ruhusa ya kutumia kiboksi hicho na kwamba kanuni mpya za ulinzi wa Mashahidi haziwezi kutumika kwa kesi iliyoanza kabla ya kutungwa kwake.

Kwa upande wa Jamhuri, Wakili wa Serikali Mkuu Nassoro Katuga aliomba kuahirishwa kwa shauri hilo ili kupata muda wa kujibu hoja za Lissu akisema hoja hizo ni nyingi na zinahitaji uchambuzi wa kina ambapo Mahakama imeahirisha usikilizwaji wa kesi hiyo hadi tarehe itakayopangwa na Msajili kwa ajili ya kuendelea na hoja za pande zote.

 

Chanzo; Millard Ayo

Kuhusiana na mada hii: