Jeshi la Polisi Mkoa wa Njombe limekanusha taarifa inayosambazwa kwenye mitandao ya kijamii, ikiwa na kichwa cha habari “Polisi Njombe achomwa moto na kuporwa silaha” kuwa hakuna tukio kama hilo mkoani humo.
Jeshi la Polisi linatoa wito kwa watu wenye tabia za kuandaa na kusambaza taarifa za uongo na upotoshaji kwa njia mbalimbali, kuacha tabia hiyo kwani kinyume cha sheria za nchi na maadili.
Chanzo; Itv