Waziri wa nchi, Ofisi ya Rais Mipango na Uwekezaji, Profesa Kitila Mkumbo asema katika mapambano dhidi ya rushwa Tanzania ni ya pili kwa Afrika Mashariki kwa kupambana na rushwa ikiwa imezidiwa na Rwanda huku Afrika, Tanzania inashika nafasi ya 14 kati ya nchi 54.
Prof. Kitila ameyasema hayo hii leo Septemba 27, 2025 katika jukwaa la Cafetalk ambapo amerejelea takwimu za Shirika la Transparency International na amesisitiza Serikali ya awamu ya sita imejidhatiti ipasavyo.
Amesema pia katika Ilani ya Chama cha Mapinduzi ni moja ya eneo muhimu katika kipengele cha utawala bora kipengele cha tatu ambacho ni kuimarisha na kuoambana dhidi ya rushwa, ufisadi, uzembe na wizi ndani ya Ofisi za Umma
“Kwenye swala la ufisadi tumefanya nini? Kwa vipimo vya Transparent International, Tanzania ni ya pili kwa Afrika Mashariki kwenye kupambana na Rushwa tumezidiwa na Rwanda, Ndani ya Afrika kati ya nchi 54 sisi ni nchi ya 14 na imeonesha kuwa tumekuwa tukipiga hatua kwenye swala hili la mapambano dhidi ya Rushwa kwa hiyo kuna kazi kubwa imefanyika ukiangalia takwimu hizi” Amesema Prof Kitila Mkumbo.
Chanzo: Millard Ayo