Jeshi la Polisi Mkoa wa Mbeya linamshikilia Tatizo Yohana Mzumbwe, mkazi wa Masoko mkoani Mbeya kwa tuhuma za mauaji ya mama yake wa kambo, Merry Yohana kwa kumkata na panga kichwani.
Taarifa ya kamanda wa Polisi mkoa wa mbeya Kamishna msaidizi mwandamizi wa polisi Benjamini Kuzaga inaeleza kwamba mtuhumiwa anadaiwa kutenda tukio hilo Oktoba 6,Kijiji cha Mapinduzi, Kata ya Masoko, Mkoani Mbeya, kwa kumuua mama huyo ambaye alikuwa mwenye ualbino na na kukimbia.
Kuzaga amesema Uchunguzi wa awali umebaini kuwa chanzo cha tukio hilo ni mgogoro wa kifamilia kuhusu mashamba ambapo mtuhumiwa alikuwa akimshinikiza Marehemu kugawa mashamba ya urithi yaliyoachwa baada ya baba yake kufariki.
Chanzo: Wasafi