Waziri Mkuu wa Tanzania Dkt. Mwigulu Nchemba leo Novemba 15, 2025 amefanya ziara ya kushtukiza katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Dodoma na kuziagiza Hospitali zote Nchini kuhakikisha Wajawazito wanapofika Hospitalini wanahudumiwa kwa haraka ili kuokoa maisha ya Mama na Mtoto.
Ametoa maagizo hayo wakati akizungumza na Wananchi nje ya Hospitali hiyo baada ya kutembelea Wananchi waliofika Hospitalini hapo kupata huduma mbalimbali za kitabibu ambapo amesisitiza Wananchi waendelee kuhudumiwa vizuri kwa kuwa Rais Dkt. Samia ametoa fedha nyingi kwa ajili ya kuboresha huduma za afya Nchini vikiwemo vifaa tiba na dawa.
Vilevile Waziri Mkuu ameziagiza hospitali zote Nchini kuhakikisha zinakuwa na vifaa vya usafi binafsi vya dharura vikiwemo ndoo na beseni katika wodi za Wazazi ili viwasaidie akinamama wasiokuwa na vifaa hivyo “Ujauzito sio suala la dharura vifaa kama ndoo tunapaswa kuwa navyo katika Hospitali zetu za Serikali.”
Dkt. Mwigulu pia alitumia nafasi hiyo kumpongeza Rais Samia akisema amefanya kazi kubwa katika uboreshaji wa huduma za afya Nchini.
Chanzo; Millard Ayo