Search

Saved articles

You have not yet added any article to your bookmarks!

Browse articles

GDPR Compliance

We use cookies to ensure you get the best experience on our website. By continuing to use our site, you accept our use of cookies, Privacy Policy, and Terms of Service.

Malori ya Tanzania Yadaiwa Kutekwa Zambia

Wamiliki wa Malori ya Kati na Madogo (Tamstoa) wamelalamikia kuongezeka kwa matukio ya kutekwa kwa malori yao na kuibiwa madini ya shaba na kopa nchini Zambia.

Balozi wa Tanzania nchini humo, Luteni Mathew Mkingule amesema ubalozi huo haujapokea taarifa rasmi kuhusu tukio lolote la aina hiyo.

Akizungumza kuhusu madai hayo, Balozi Mkingule amesema endapo matukio ya wizi au utekaji yametokea, wahusika wanapaswa kwanza kutoa taarifa kwa vyombo vya usalama vya Zambia, hususan Jeshi la Polisi, ili uchunguzi uanze.

Amefafanua kuwa baada ya Polisi kupokea taarifa, ndipo wanapaswa kuwasiliana na Ubalozi wa Tanzania ili kutoa taarifa endapo kuna raia wa Tanzania aliyehusika au kuathiriwa.

“Wamiliki wa magari au wasafirishaji wanapaswa pia kuwasiliana na ubalozi ili kuanza mchakato wa ufuatiliaji. Hizi ndizo taratibu rasmi, sawa na ilivyo Tanzania ambapo tukio la wizi lazima liripotiwe Polisi kwanza,” amesema Mkingule.

Akieleza sababu za kuvunja ukimya wao, Dar es Salaam jana Januari 15, 2026 Mwenyekiti wa Tamstoa, Chuki Shabani, amedai vitendo vya kutekwa kwa malori yanayobeba shaba na kopa kutoka Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC) kwenda Tanzania vimekithiri.

 

 

 

Chanzo; Mwananchi

Kuhusiana na mada hii: