Search

Saved articles

You have not yet added any article to your bookmarks!

Browse articles

GDPR Compliance

We use cookies to ensure you get the best experience on our website. By continuing to use our site, you accept our use of cookies, Privacy Policy, and Terms of Service.

Petroli Bei Juu, Dizeli na Mafuta ya Taa Kicheko

Watumiaji wa vyombo vya moto vinavyotumia petroli wataendelea kuugulia maumivu ya ongezeko la bei katika mafuta katika mwezi Februari 2026 huku watumiaji wa dizeli na mafuta ya taa kicheko.

Hiyo ni baada ya petroli kuendelea kupanda kwa mujibu wa bei kikomo zilizotolewa na Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji ( Ewura) zitakazotumika kuanzia leo Februari 4, 2026.

Ongezeko la bei ya petroli nchini inashuhudiwa wakati ambao bei kikomo kwa Februari 2026 za mafuta hayo katika soko la dunia zimepungua kwa asilimia 6.41, asilimia 0.50 kwa mafuta ya dizeli na asilimia 1.70 kwa mafuta ya taa.

Licha ya bei ya mafuta kupungua kwenye soko la dunia katika mwezi husika gharama za kuagiza mafuta katika Bandari ya Dar es Salaam zimeongezeka kwa wastani wa asilimia 1.88 kwa mafuta ya petroli na asilimia 1.65 kwa mafuta ya taa na kupungua kwa wastani wa asilimia 5.10 kwa mafuta ya dizeli.

Katika bandari ya Tanga zimepungua kwa asilimia 1.62 kwa petroli na dizeli na katika bandari ya Mtwara zimepungua kwa asilimia 9.24 kwa mafuta ya petroli na hakuna mabadiliko kwenye mafuta ya dizeli.

 

 

Chanzo; Mwananchi

Kuhusiana na mada hii: