Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Balozi Dkt. Emmanuel Nchimbi amesema Serikali inayoongozwa na Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan imechukua hatua za kurejesha utengamano katika nchi na kuhakikisha wananchi wanaishi katika utawala wa sheria.
Makamu wa Rais amesema hayo wakati akimwakilisha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan katika Mkutano wa Dharura wa Wakuu wa Nchi na Serikali wa Nchi Wanachama wa Jumuiya ya Maendeleo Kusini Mwa Afrika (SADC), uliyofanyika kwa njia ya mtandao, akiwa mkoani Dodoma na kueleza kuwa serikali itaanzisha mazungumzo ya maridhiano.
Chanz; Global Publishers