Jeshi la Polisi mkoani Mtwara linachunguza tukio la jaribio la mauaji linalomhusisha mtoto Shaban Muebo (12), mkazi wa Kijiji cha Masyalele, Wilaya ya Nanyumbu, anayedaiwa kujaribu kumuua mtoto mwenzake, Ibrahimu Salumu (4).
Akizungumza na waandishi wa habari, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mtwara, Issa Suleiman, amesema tukio hilo lilitokea Januari 23, 2026.
Amesema mtuhumiwa anadaiwa kumlaghai mtoto huyo aliyekuwa anacheza na wenzake na kumchukua hadi katika Msitu wa Jando uliopo kijijini hapo, ambako alimjeruhi shingoni kwa kutumia wembe kisha kumtelekeza katika msitu huo.
Kwa sasa, mtoto aliyejeruhiwa anaendelea kupatiwa matibabu katika Hospitali ya Misheni Ndanda, huku Jeshi la Polisi likiendelea na uchunguzi wa tukio hilo.
Chanzo; Bongo 5