Baada ya idara ya vijana kuwa idara ndani ya wizara Rais wa Jamhuri wa Muungano wa Tanzania asema wamefikiria kuja na wizara inayoshighurikia mambo ya vijana.
Ameweka wazi hayo yote wakati akilihutubia Bunge la 13, Novemba 14, Dodoma.
"Serikalini tumefikiria kuwa na wizara kamili itakayoshughulika na mambo ya vijana, tumeamua kuwa na wizara kamili badala ya kuwa na idara ndani ya wizara yenye mambo mengi.”
“Nafikiria kuwa na washauri wa mambo ya vijana ndani ya ofisi ya rais, jambo jingine tulilofikiria ni kuchukua hatua ya kuongeza mitaji kwa ajili ya shughuli za kiuchumi za vijana na wanawake kwa kutenga bilioni 200.” - Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Chanzo; Tanzania Journal