Search

Saved articles

You have not yet added any article to your bookmarks!

Browse articles

GDPR Compliance

We use cookies to ensure you get the best experience on our website. By continuing to use our site, you accept our use of cookies, Privacy Policy, and Terms of Service.

Wanawake Waibua Mjadala Umiliki Ardhi ya Ukoo

Masuala ya kisera, ikiwamo ajenda ya wanawake kuruhusiwa kumiliki ardhi ya ukoo, biashara ya hewa ukaa na namna Sera ya Taifa ya Ardhi ya mwaka 1995, Toleo Jipya la 2023, inavyoshughulikia haki za makundi mbalimbali, yameibua mjadala mkali katika jumuiko la mashirika 14 nchini.

Majadiliano hayo yamefanyika Februari 13, 2026 katika kituo cha SOS Children’s Villages kilichopo Ngaramtoni mkoani Arusha, yakilenga kuchambua utekelezaji wa Sera ya Taifa ya Ardhi ya Mwaka 1995 Toleo Jipya la 2023 iliyozinduliwa Machi 17, 2025 na Rais Samia Suluhu Hassan.

Akizungumza katika jukwaa hilo, Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Utafiti na Utetezi wa Haki Ardhi, Cathbert Tomitho, amesema ardhi ni rasilimali kuu ya Taifa kwa kuwa zaidi ya asilimia 74 ya Watanzania wanaishi vijijini ambako huzalishwa chakula kwa matumizi ya ndani na kwa ajili ya mauzo nje.

Ameeleza kuwa pamoja na umuhimu wa ardhi katika kilimo, utalii, misitu na uwekezaji, bado kuna maswali kuhusu namna sera hiyo inavyolinda haki za wanawake, watoto wa kike, watu wenye ulemavu, wakulima na wafugaji.

“Hoja yetu kubwa ni kuona sheria zitakazofuata baada ya sera kuweka mikakati ya kulinda ardhi ya vijiji dhidi ya uwekezaji mkubwa na migogoro, na kuhakikisha wanawake na makundi mengine wananufaika kwa haki,” amesema Tomitho.

Katika mjadala huo, Wakili Valentina Clifford, Ofisa Mipango Mwandamizi wa Taasisi ya Haki Ardhi, amesema sera imeshindwa kuweka takwimu zilizotenganishwa kijinsia (gender disaggregated data) kuhusu umiliki wa hati za kimila.

“Sera inataja idadi ya hati zilizotolewa, lakini haijaweka bayana ni wanawake wangapi na wanaume wangapi wanamiliki ardhi. Bila takwimu hizo, inakuwa vigumu kusukuma usawa wa kijinsia katika umiliki wa ardhi,” amesema.

 

 

 

Chanzo; Nipashe

Kuhusiana na mada hii: