Search

Saved articles

You have not yet added any article to your bookmarks!

Browse articles

GDPR Compliance

We use cookies to ensure you get the best experience on our website. By continuing to use our site, you accept our use of cookies, Privacy Policy, and Terms of Service.

Azma ya Rais Samia kwa Kardinal Pengo

Makamu wa Rais, Balozi Emmanuel Nchimbi ameeleza namna Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. Samia Suluhu Hassan alivyoridhia kutoa ndege ya huduma za dharura kwa wagonjwa ili kufanikisha safari ya Mwadhama Polycarp Kardinali Pengo kurejea nchini.

‎Dk. Nchimbi amefichua siri hiyo leo, Jumamosi Februari 28,2026 wakati akitoa salamu katika mazishi Kardinali Pengo yatakayofanyika Kituo cha Hija kilichopo Pugu jijini Dar es Salaam.

‎Ameeleza kuwa kuanzia Februari 12-15, Rais Dk. Samia alisafiri kikazi nchini Ethiopia na kwa utaratibu wa Katiba ya Tanzania, mamlaka ya urais alikabidhiwa yeye.

‎“Akiwa angani (Dk. Samia) ndipo nilipoletewa taarifa kuhusu hali ya Kardinali Pengo imebadilika, lakini alisisitiza kuwa chochote kitakachoweza kutokea kwake atafarijika kikitokea akiwa ndani ya ardhi ya Tanzania,” ameleeza Dk. Nchimbi.

‎Dk. Nchimbi anasema alipoombwa kusaidia ufanikishaji baada ya kuelezwa changamoto ya usafiri, alidhani ni jambo dogo kwa kuwa alikabidhiwa mamlaka na Rais Samia.

‎“Niliwasiliana na wenzangu akiwamo Waziri Mkuu, baadaye nilijua ni habari ya kubadilisha tiketi tu haraka haraka, ilipokuja taarifa kuwa kwa hali yake namna ya kumrudisha nyumbani (Pengo) kwa muda anaotaka yeye kuwahi lazima kukodi ndege ya ‘ambulance’,”

‎“Sasa hapo kwenye ndege ya ambulance hayo madaraka ya kurithi yalitaka kunitokea puani, washauri wakanielez kwa hatua hiyo lazima Rais afanye uamuzi.Nikamwandikia Rais ujumbe mrefu, akanijibu ameridhia ufanyike mchakato haraka sana,”

‎Balozi Nchimbi amesema pamoja na heshima kubwa ambayo Rais Dkt Samia ameitoa kwa Kardinali Pengo kwa kutambua mchango wake kwa Tanzania, lakini inatoa hamasa kwa Watanzania wengine wasio viongozi wa siasa kuonesha mapenzi kwa Taifa lao.

 

 

Chanzo; Nipashe

Kuhusiana na mada hii: