KUMRADHI:** Tunapenda kusahihisha taarifa tuliyoichapisha mapema leo Ijumaa kuhusu ripoti mpya iliyotolewa nchini Tanzania juu ya hasara ya kiuchumi iliyopatikana kwa kuzimwa au kutatizwa kwa huduma ya intaneti wakati na baada ya uchaguzi wa mwaka uliopita.
Ripoti hiyo ya mwaka 2025 iliyoandaliwa na asasi kadhaa zinazounda taasisi ya kufuatilia mwenendo wa huduma za intaneti nchini Tanzania na kuratibiwa na kampuni ya Tech & Media Convergency (TMC), inaonesha hasara ya kutatizwa mawasiliano ya intaneti mwaka uliopita ilikuwa dola za kimarekani milioni 238 sawa na shilingi za kitanzania bilioni 560.
Kwa mujibu wa ripoti hiyo, hasara ya kuzimwa huduma za intaneti kwa siku 5 pekee kuanzia siku ya uchaguzi Oktoba 29 hadi Novemba 03, 2025, ilifikia dola milioni 72.3 sawa na shilingi bilioni 185 za Tanzania.
Hasara hiyo imetokana na kutatizika kwa huduma za kutuma na kupokea fedha kwa njia ya benki na mitandao ya simu na rikodi ya stakabadhi za kikodi.
Chanzo; Dw