Search

Saved articles

You have not yet added any article to your bookmarks!

Browse articles

GDPR Compliance

We use cookies to ensure you get the best experience on our website. By continuing to use our site, you accept our use of cookies, Privacy Policy, and Terms of Service.

Polisi Wajibu Polepole Kutekwa “Bado Tunamsubiri”

Baada ya picha mjongeo kadhaa kusambaa ndani ya mitandao ya kijamii Oktoba 6,2025 ikiwemo iliyobeba taarifa ya mtu aliyejitambulisha kuwa kaka yake Humphrey Polepole na kudai kuwa ametekwa.

Jeshi la Polisi Tanzania limetoka hadharani kujibu kinachoendelea mtandaoni dhidi ya tukio hilo ambapo limesema bado linaendela kumsubiri Polepole aripoti kituo cha Polisi.

“Jeshi la Polisi linaependa kutoa taarifa kwamba, bado linaendelea kumsubiri Ndg. Humphrey Polepole aripoti katika Ofisi ya Mkurugenzi wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai ili atoe maelezo kuhusu na tuhuma mbali mbali alizozitoa kupitia Mitandao ya Kijamii lakini hadi leo hajatekeleza maelekezo hayo kwa mujibu wa Sheria.”

Zaidi “Taarifa zinazosambazwa kwenye Mitandao ya Kijamii na ndugu zake kuwa ametekwa, tayari tumeanza kufanya kazi za taarifa husika ili kupata ukweli wake.”

Ikumbukwe, Septemba 15,2025, Jeshi la Polisi lilimtaka Polepole, afike kituo cha Polisi kwa ajili ya kutoa ushuhuda dhidi ya tuhuma ambazo amekuwa akizitoa mtandaoni.

Chanzo: Tanzania Journal

Kuhusiana na mada hii: