Search

Saved articles

You have not yet added any article to your bookmarks!

Browse articles

GDPR Compliance

We use cookies to ensure you get the best experience on our website. By continuing to use our site, you accept our use of cookies, Privacy Policy, and Terms of Service.

Watoto Kupewa Vileo Sababu ya Ongezeko la Udumavu Iringa

Wakati kiwango cha udumavu nchini Tanzania kikiwa juu ya wastani wa dunia wa asilimia 22, Mkoa wa Iringa ni miongoni mwa mikoa yenye viwango vya juu zaidi, ikiwa na asilimia 56.9, licha ya kuwa miongoni mwa wazalishaji wakubwa wa chakula nchini.

Kulea watoto maeneo ya kazi na kuwapa vileo walio chini ya umri wa miaka mitano kumechangia kuwepo kwa kiwango hiki kikubwa cha udumavu miongoni mwa watoto mkoani Iringa, uchunguzi wa Mwananchi umebaini.

Iringa ina idadi kubwa ya watoto waliodumaa chini ya umri wa miaka mitano, licha ya kuwa miongoni mwa mikoa inayozalisha chakula kwa wingi nchini Tanzania.

Watoto huchukuliwa kuwa wamedumaa iwapo urefu wao, kulingana na umri, uko chini kwa zaidi ya viwango viwili vya kawaida ikilinganishwa na wastani uliowekwa na Shirika la Afya Duniani (WHO).

Sababu za udumavu ni lishe duni kabla na wakati wa ujauzito, katika hatua za awali za utoto, maambukizi ya mara kwa mara, pamoja na ukosefu wa msisimko wa kisaikolojia, hali inayoathiri ukuaji na maendeleo ya mtoto.

Takwimu za Utafiti wa Afya ya Uzazi na Mtoto Tanzania wa mwaka 2022 (TDHS-MIS) zinaonesha kuwa udumavu unaathiri asilimia 56.9 ya watoto chini ya miaka mitano mkoani Iringa, ukifuatiwa na Njombe kwa asilimia 50.4 na Rukwa kwa asilimia 49.8. Kati ya watoto waliodumaa Iringa, asilimia 17.3 wameainishwa kuwa na kiwango kikubwa cha udumavu.

 

 

Chanzo; Mwananchi

Kuhusiana na mada hii: