Search

Saved articles

You have not yet added any article to your bookmarks!

Browse articles

GDPR Compliance

We use cookies to ensure you get the best experience on our website. By continuing to use our site, you accept our use of cookies, Privacy Policy, and Terms of Service.

Heka 1 ya Parachichi Mkulima Anapata Dola 7000

Mbunge wa Bunda Mjini, Ester Bulaya amesema endapo Serikali itaamua kujifunga mkanda na kuwekeza katika Sekta ya Kilimo cha umwagiliaji kwa kuziunganishia mifumo ya umwagiliaji hekari milioni tano kwa mwaka kipato cha mkulima mmoja mmoja kitakuwa na pia kukuza pato la Taifa.

Akichangia Mpango Elekezi wa Maendeleo wa Muda Mrefu (2026/27–2050/51), Mpango wa Nne wa Maendeleo wa Taifa wa Miaka Mitano (2026/27–2030/31) pamoja na Mapendekezo ya Mpango wa Maendeleo wa Taifa wa Mwaka 2026/27, Bulaya amesema ni lazima serikali ibadilishe fikra za watendaji wake ili maeneo hayo yawe na tija ya kiuchumi.

“Msheshimiwa Waziri tuna hekari milioni 29.4 zinazofaa kwa kilimo cha Umwagiliaji, leo hekta ambazo zimeunganishwa na mfumo wa umwagiliaji ni hekari laki saba peke yake na mmeona mwaka huu tumekumbwa na tishio la hali ya hewa ya mvua, hivi leo tukiamua kuwekeza kwenye sekta ya kilimo cha Umwagiliaji tukasema tunafunga mkanda tukasema tuna anza na Hekta milioni Tano kwa wakulima wadogo wadogo kuunganishiwa mfumo wa umwagiliaji tutaongeza pato letu lakini tutakuwa na uhakika wa kulima kutoka msimu mara moja mpaka msimu mara mbili.” Amesema Ester Bulaya.

 

 

Chanzo; Millard Ayo

Kuhusiana na mada hii: