Search

Saved articles

You have not yet added any article to your bookmarks!

Browse articles

GDPR Compliance

We use cookies to ensure you get the best experience on our website. By continuing to use our site, you accept our use of cookies, Privacy Policy, and Terms of Service.

Pingamizi la Lissu Mahakama Yalitupilia Mbali

Mahakama Kuu, Masjala Ndogo Dar es Salaam, imetupilia mbali pingamizi la Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Tundu Lissu, katika kesi ya uhaini inayomkabili.

 

Katika uamuzi huo uliotolewa leo, Jumatatu, Septemba 15, 2025, Mahakama imeitupilia mbali hoja za Lissu, huku ikisema ina mamlaka ya kuisikiliza kesi hiyo

“Mahakama baada ya kupitia hoja za pande zote imeridhika kuwa mapingamizi haya hayawezi kuharibu mwenendo mzima wa Mahakama ya Ukabidhi na kuifanya Mahakama hii kukosa mamlaka. Hivyo sababu hii ya pingamizi inakataliwa,” amesema Jaji Dunstan Ndunguru (kiongozi wa jopo) wakati akisoma uamuzi huo baada ya kujadili hoja zote.

 

Kwa mujibu wa gazeti la Mwananchi, katika pingamizi lake hilo, Lissu alidai kuwa Mahakama hiyo (Mahakama Kuu) haina mamlaka ya kusikiliza kesi hiyo huku akibainisha hoja saba. Hoja hizo alizodai zinaifanya Mahakama hiyo kukosa mamlaka ya kusikiliza kesi hiyo ni pamoja na ubatili wa mwenendo kabidhi na mamlaka ya Mahakama ya Ukabidhi.

 

Kwa uamuzi huo, Mahakama hiyo imepanga kuendelea na usikilizaji wa sababu ya pili ya pingamizi la Lissu, inayohusu uhalali wa hati ya mashtaka leo hii.

Tundu Lissu aliwasilisha mapingamizi mawili. Pingamizi la kwanza, ambalo tayari limesikilizwa, linahusu mamlaka ya Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam kusikiliza kesi yake, huku Lissu akidai kuwa Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu haikuwa na mamlaka ya kisheria kuendesha mchakato wa awali. Pingamizi la pili litasikilizwa baada ya Mahakama kutoa uamuzi juu ya pingamizi la kwanza; linalenga hoja yake kwamba Hati ya Mashitaka iliyotolewa Kisutu ni mbovu kisheria, haiwezi kuendelea bila marekebisho.

Katika hoja zake, Lissu ameibua hoja tano kuu:

·         Mahakama ya Kisutu haikuwa na mamlaka ya kisheria kusikiliza kesi.

·         Mashitaka yanayomkabili Lissu ni ya kisiasa na hayana msingi wa kisheria.

·         Hukumu ya awali na machakato wake wote katika Mahakama ya ukabidhi (Kisutu) haipaswi kuendelea kuwa na nguvu ya kisheria.

·         Ana haki ya msingi ya kikatiba ya usikilizaji wa haki bila masharti.

·         Anaomba kesi ifutwe mara moja na kuachiliwa huru bila masharti yoyote.

Ikumbukwe, Tundu Lissu alikamatwa Aprili 9, 2024, Mimba na kupelekwa Dar es Salaam. Siku iliyofuata, Aprili 10, 2024, alishitakiwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu. Lissu anapinga hatua hii akisema ni kinyume cha sheria, kwa sababu sheria inataka mashitaka yapelekwe kama hatua za kisheria za kukamata mtu na kesi iendelewe katika mahakama yenye mamlaka halali.

 

Nyaraka za mwenendo wa kesi hazikukamilika kikamilifu; nyaraka zilizotolewa zenye mapungufu ziliibua pingamizi la Lissu. Kwa mfano, alipatiwa nyaraka za Agosti 18, 2025, ambazo ni page 116 badala ya page 103 za mchakato mzima, jambo ambalo alidai linaonyesha mapungufu na makosa yanayoweza kumzuia haki na kutikisa haki za kisheria. Lissu anaamini kuwa makosa hayo yanayohusiana na mamlaka ya Mahakama ya Kisutu yanazuia hata Mahakama Kuu kuendelea na shauri bila kuangalia pingamizi lake.

 

Anakabiliwa na shitaka la uhaini kinyume na kifungu cha 39(2)(d) cha Sheria ya Kanuni za Adhabu, kilichotokana na maneno aliyoyatamka yanayohusiana na mpango wa kudhibiti au kuzuia uchaguzi mkuu wa 2025. Mashitaka haya yamevutia umakini mkubwa wa umma na vyombo vya habari, huku wananchi wengi wakisubiri kwa hamu uamuzi wa Mahakama Kuu: kuachiwa huru au kuendelea kusota rumande, jambo linaloangaliwa kuwa na athari kubwa kisiasa na kisheria nchini Tanzania.

 

 

Chanzo; Bbc Swahili

Kuhusiana na mada hii: