Askari 15 wa jeshi la polisi mkoa wa Mbeya wenye vyeo mbalimbali wametunukiwa tuzo za sifa na zawadi kwa kufanikisha kuwanasa wahalifu Hatari waliotekeleza matukio mbalimbali ya uhalifu yanayoigusa jamii ikiwemo mauaji, Ubakaji, uuzaji na usafirishaji wa dawa za kulevya.
Tuzo hizo zimetolewa Kwenye kikele cha siku ya familia ya polisi mkoa wa Mbeya, ambapo Mkuu wa mkoa wa huo Mhe Beno Malisa, anasema pamoja na askari hao kufanya vizuri kwenye dawati la jinsia bado kuna kazi kubwa ya kufanya hasa kudbiti matukio ya ubakaji na ulawiti ambayo kwa sasa yamekua yakiripotiwa kufanyika zaidi kwenye ngazi ya familia.
Kamanda wa polisi mkoa wa Mbeya Kamishna msaidizi mwandamizi wa Polisi Benjamini Kuzaga, anaeleza namna watakavyo lifanyiakazi jambo hilo ili kupunguza na kumaliza kabisa matukio ya ukatili wa kijinsia, Huku baadhi ya Askari waliotunukiwa tuzo hizo wakiadi kuendelea na mapambana ya ukatili kwa watoto huku wakiiomba jamii kushiriki kwa kutoa taarifa.
Chanzo; Wasafi