Mahakama kuu ya Tanzania masijala ndogo ya Dar es salaam imeamuru mshatakiwa wa kesi ya uhaini Tundu Lissu ambaye pia ni mwenyekiti wa chama cha upinzani CHADEMA kufikishwa mahakamani tarehe 12/11/2025 siku ya Jumatano
Hii leo Jumatatu tarehe 10/11/2025 hakufikishwa mahakamani kwa kile upande wa waleta mashitaka (Jamuhuri) kudai hajafikishwa mahakamani kutokana na hali ya kiusalama katika Jiji la Dar es salaam baada ya ghasia za uchaguzi,
Mashahidi wa Lissu na wa Jamuhuri nao pia hawakufika mahakamani kwa sababu hizo hizo na mahakama imeamuru wajiandae na wafike mahakamani siku iliyoelekezwa ili kuweza kuendelea na shauri hilo.
Chanzo; Bbc