Mwanamke mmoja anayejulikana kwa jina la Hadija Jimmy, mkazi wa Manispaa ya Tabora, anashikiliwa na Jeshi la Polisi mkoani humo kwa tuhuma za kujiteka ili apate fedha kutoka kwa baba wa mtoto wake.
Akizungumza na waandishi wa habari, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Tabora, SACP Richard George Abwao, amesema jeshi hilo linawashikilia watu watatu kwa tuhuma za kufanikisha mpango huo.
Chanzo; Global Publishers