Rais Samia Suluhu Hassan ametangaza baraza jipya la mawaziri Novemba 17,2025 Ikulu ya Chamwino, Dodoma.
Baraza hilo linajumuisha sura mpya na waliowahi kushika nafasi za juu serikalini, ikilenga kuongeza kasi ya utendaji na uwajibikaji wa serikali ya awamu ya sita.
Hii ni orodha ya baadhi ya majina yaliyotajwa katika baraza jipya:
• Dkt. Mwigulu Nchemba – Waziri Mkuu
• Balozi Dkt. Bashiru Ally Kakurwa – Waziri wa Mifugo na Uvuvi
• Anthony Peter Mavunde – Waziri wa Madini
• Deogratious John Ndejembi – Waziri wa Nishati
• Juma Zuberi Homera – Waziri wa Katiba na Sheria
• Prof. Palamagamba John Kabudi – Waziri wa Habari, Sanaa na Michezo
• Dkt. Ashatu Kachwamba Kijaji - Waziri wa Maliasili na Utalii
• Dkt. Leonard Douglas Akwilapo – Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi
• Prof. Adolf Faustin Mkenda – Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia
• Mohamed Omary Mchengerwa – Waziri wa Afya
• Dkt. Dorothy Onesphoro Gwajima – Waziri wa Maendeleo ya Jamii
• Angela Mbelwa Kariuki – Waziri wa Mawasiliano na Teknolojia ya Habari
• Judith Salvio Kapinga – Waziri wa Viwanda na Biashara
• Prof. Makame Mbarawa Mnyaa – Waziri wa Uchukuzi
• Abdallah Hamis Ulega – Waziri wa Ujenzi
• Dkt. Rhimo Simeon Nyansaho - Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa
Chanzo; Dw