Mfanyabiahara Jenifer Jovin (Niffer) na wenzake 21 wamesomewa mashtaka matatu (3) ya uhaini
Kosa la kwanza linalowahusu washtakiwa wote 22 ambapo ni kwamba kwa pamoja wamekula njama ya kutenda kosa au kupanga uhalifu ambao ni uhaini
Kosa la pili ambalo ni la uhaini linawahusu washtakiwa 21 isipokuwa mshtakiwa mmoja pekee ambaye ni Niffer,
ambapo washtakiwa walianzisha nia ya kuzuia uchaguzi Mkuu 2025, na kutishia mamlaka na wakatekeleza nia hiyo kwa kufanya vurugu zilisababisha uharibifu wa mali za umma,
Na kosa la tatu la uhaini pia linamuhusu mshtakiwa namba moja pekee ambaye ni Niffer,
ambapo alihamasisha watu kuvuruga uchaguzi Mkuu 2025 na kuhamasisha umma kununua barakoa za kuzuia mabomu ya machozi kutoka dukani kwake
Chanzo; Wasafi Media