Shirika la Mandeleo la Viwanda Vidogo (SIDO) limetenga maeneo ya viwanda 25 yatakayowawezesha vijana kupata maeneo ya kufanya kazi za uzalishaji kwa kutumia mitaa ya viwanda na kongani.
Hatua hiyo ni sehemu ya utekelezaji wa ahadi za Rais Samia Suluhu Hassan alizozitoa wakati wa kampeni za Uchaguzi Mkuu, ndani ya siku 100.
Mkurugenzi wa Teknolojia na Maendeleo ya Viwanda, Mhandisi Benedictor Kalumuna ameeleza hayo leo Februari 04 wakati wa uzinduzi wa maeneo hayo.
Mhandisi Kalumuna alimwakilisha Mkurugenzi Mkuu wa SIDO, Profesa Silvester Mpanduji.
Akiwa katika uzinduzi huo, amesema licha ya juhudi zinazofanywa na serikali za kujenga mitaa ya viwanda bado wadau wanahitajika katika kusukuma gurudumu la vijana na kuleta maendeleo ya nchi.
Chanzo; Nipashe