Katika kuwasilisha ujumbe wa Mhe Rais Dkt.Samia Suluhu Hassan Waziri wa mambo ya nje na ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe Balozi Kombo amemuomba Baba Mtakatifu aombee amani nchini Tanzania baada ya maafa yalijitokeza katika uchaguzi Mkuu 2025
Kiongozi wa Kanisa Katoliki Duniani, Papa Leo XIV, ameahidi kuiombea Tanzania amani na utulivu, baada ya maafa ya Oktoba 29, mwaka jana, huku akidokeza amewahi kuishi nchini katika mikoa ya Morogoro, Dar es Salaam, Ruvuma na Arusha.
Balozi Kombo amekutana na Papa Leo XIV, leo Jumatano Januari 28, 2026 saa chache kabla ya Katekesi ya kiongozi huyo wa kiroho Vatican.
Katika hatua nyingine, Balozi Kombo na ujumbe wake ulikutana na Waziri wa Mambo ya Nje wa Vatican, Askofu Mkuu, Paul Gallagher, ambaye pamoja na mambo mengine amewasilisha wito rasmi kutoka kwenye Ukulu Mtakatifu kwa Tanzania kufungua ubalozi Vatican. Kwa sasa Tanzania inawakilishwa kutokea Ujerumani
Chanzo; Eatv