Search

Saved articles

You have not yet added any article to your bookmarks!

Browse articles

GDPR Compliance

We use cookies to ensure you get the best experience on our website. By continuing to use our site, you accept our use of cookies, Privacy Policy, and Terms of Service.

Wasimamishwa Kazi kwa Matumizi Mabaya ya Ofisi

Watumishi wawili wa Halmashauri ya Wilaya ya Mkalama, mkoani Singida ambao ni Afisa Utumishi na Mhandisi wa Halmashauri hiyo wameelekezwa kusimamishwa kazi ili kupisha uchunguzi wa tuhuma za matumizi mabaya ya ofisi na ubadhirifu wa fedha za miradi ya maendeleo.

Agizo hilo limetolewa na Naibu Waziri, Ofisi ya Waziri Mkuu – TAMISEMI anayeshughulikia Elimu, Mhe. Reuben Kwagilwa (Mb), kwa niaba ya Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu – TAMISEMI, Mhe. Prof. Riziki Shemdoe (Mb), wakati wa ziara ya kikazi ya kukagua miradi ya elimu na barabara wilayani humo.

Mhe. Kwagilwa amesema Afisa Utumishi bw. Eliah Noah Samata amekuwa kikwazo kwa utendaji wa watumishi wengine kutokana na kushindwa kutimiza majukumu ya msingi ya kusimamia rasilimali watu, hali inayochochea uzembe kazini na kuchelewesha utoaji wa huduma kwa wananchi.

Kwa upande wa Mhandisi wa Halmashauri hiyo, Bw. Innocent Magadula, amebainika kusimamia vibaya mradi wa ujenzi wa shule mpya ya msingi katika eneo la Shule ya Sekondari Grace Mesaki. Ametuhumiwa kuruhusu matumizi ya vifaa visivyokidhi viwango, ikiwemo kutumia changarawe badala ya mawe maalum katika sakafu za madarasa, hatua inayohatarisha uimara wa majengo na usalama wa wanafunzi.

Imebainika pia kuwa baadhi ya vipimo vya ujenzi vilivyokuwa kwenye makisio ya gharama (BOQ) vilipunguzwa bila kufuata taratibu, jambo linalokiuka miongozo ya Serikali na kuonyesha uzembe mkubwa katika usimamizi wa miradi ya maendeleo.

 

 

Chanzo; Clouds Media

Kuhusiana na mada hii: