Halmashauri ya Wilaya ya Tunduru imejipanga kuajiri watumishi wa kujitolea kwa mkataba 172 wakiwemo walimu 100 katika Idara ya Elimu ya awali na msingi pamoja na wengine 16 wa idara ya elimu ya sekondari.
Imeelezwa kuwa watumishi wengine 56 wataelekezwa sekta ya Afya, na kwamba hatua hiyo inayolenga kupunguza uhaba wa watumishi na kuboresha utoaji wa huduma kwa wananchi.
Mpango huo umeidhinishwa Febbruari 15, mwaka huu katika kikao maalum cha baraza la madiwani kilichofanyika Tunduru kupitisha rasimu ya mpango wa bajeti kwa mwaka wa fedha 2026/2027 ikiwa ni takribani Sh. Bilioni 55.04.
Akiwasilisha rasimu hiyo ya bajeti kwa niaba ya Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri, Ofisa Mipango Bosco Mwingira, amesema kupitia mapato ya ndani ya halmashauri hiyo imeweka msisitizo katika kuimarisha sekta za elimu na afya kwa mwaka wa fedha 2026/2027.
Chanzo; Nipashe